
Simone Inzaghi kocha mpya wa Inter Milan
Inzaghi amejiunga na timu hiyo akitokea timu ya Lazio, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Antonio Conte aliyeondoka klabuni hapo wiki moja iliyopita baada ya kuwapa ubingwa wa msimu wa 2019/2020.
Inzaghi ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa vilabu vya Lazio , Sampodoria Atalanta na timu ya Taifa ya Italia iliitengeneza timu hii na kuifanya kuwa shindani katika msimu huu wa serie A
Mafanikio yake akiwa na Lazio msimu huu, ni kumaliza katika nafasi ya 6 msimamo wa serie A akiwa ameshinda michezo 21 kati ya 38 imesare 5 na kupoteza 12 imemaliza ikiwa na alama 68 .