Jumanne , 4th Feb , 2020

Klabu ya Simba imethibitisha kupokea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ya kiungo, Shiza Kichuya baada ya kuisubiri kwa taribani mwezi mmoja.

Kikosi cha Simba

Simba imesema kuwa Kichuya sasa anaweza kutumika katika mchezo wowote endapo kocha ataamua kumtumia.

Wachezaji wawili wa Simba, Shiza Kichuya na Luis Miquissone walikuwa wakisubiria ITC zao kwa ajili ya kuanza kuitumikia klabu yao mpya, ambapo hivi sasa Luis Miquissome ndiye aliyesalia kwani hati zake hazijawasili.

Katika taarifa ya klabu, jana Februari 4, ilieleza kuwa ITC ya Miquissome haijawasili ambapo wanahitaji maamuzi ya Kamati ya Hadhi za Wachezaji ya FIFA, baada ya kuitaka Simba ipeleke maelezo ya usajili wake.

Leo, saa 1 Usiku, Simba inashuka dimbani katika Uwanja wa Taifa kucheza na Polisi Tanzania, huku ikiwa kileleni mwa ligi kwa jumla ya pointi 47.