Jumatano , 12th Dec , 2018

Kikosi cha Simba kimesafiri leo alfajiri kuwafuata Nkana Red Devils ya nchini Zambia tayari kwa mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya Klabu Bingwa Afrika wikiendi hii.

Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuanza safari

Kikosi hicho kimeongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Francis Ndulane pamoja na wachezaji 20, watu sita kutoka benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Patrick Aussems na viongozi watatu wa klabu.

Kikosi cha Simba kilichopaa kuelekea nchini Zambia ni:

Makipa: Aishi Manula, Deo Munishi Dida.

Mabeki: Nicholas Gyan, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Juuko Murshid.

Viungo: Jonas Mkude, James Kotei, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Haruna Niyonzima, Rashid Juma, Shiza Kichuya.

Washambuliaji: John Bocco, Emmanuel Okwi, Adam Salamba, Meddie Kagere.

Baada ya mchezo huo ambao utapigwa Jumamosi, Simba itarejea nchini kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa marudio. Endapo Simba itavuka hatua hii ya pili, itafuzu hadi hadi hatua ya makundi ya michuano hiyo, ambapo itakuwa ni historia kubwa kwa klabu hiyo baada ya miaka mingi kupita.