
Ronald Koeman
Kwa mujibu wa Rais wa Barcelona, Joan Laporta ni kwamba Koeman ameondoshwa na atazungumza na wachezaji leo na ni sehemu ya kuwaaga baada ya kuhitimisha kazi yake.
Koeman raia wa Uholanzi amefutwa kazi muda mchache baada ya kufungwa na Rayo Vallecano bao 1-0 na kuifanya Barcelona iporomoke had nafasi ya 9 katika msimamo wa La Liga.
Kocha huyo anaondolewa baada ya kutumikia Barcelona kwa miezi 14, lakini ameandamwa na matokeo mabaya msimu huu ambapo amekusanya alama 15 pekee katika mechi 10 za Ligi Kuu ya Hispania na michezo minne ya mwisho amepoteza mitatu huku akichagizwa na kipigo katika El Classico dhidi ya Real Madrid.
Koeman amekutana na changamoto kubwa ambapo klabu inapitia kipindi kigumu cha kiuchumi,na kikubwa alichokifanya ni kuifanya Barcelona kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu msimu uliopita na pia kutwaa kombe la Mfalme.
Alijiunga na Barcelona mnamo Agosti, 2020 a#baada ya kurejeshwa na aliyekuwa Rais wa Klabu hiyo Maria Bartomeu na sasa Xavi Hernandez ambaye kwa sasa ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake.