Kyrie Irving akiwa dimbani
Irving alifunga alama 22 ndani ya dakika 32 alizocheza na kuisaidia Nets kurejea kwenye mbio za ubingwa huku akizungukwa na wachezaji wa daraja la juu kama Kevin Durant na James Harden.
Mchezaji huyo wa zamani wa Cleveland Cavaliers alikuwa nje kutokana na kutochoma chanjo ya UVIKO-19 ambapo mpaka sasa bado hajachoma na hivyo kumlazimu kucheza kwenye majimbo ambayo hayana vizuizi vya UVIKO-19 kwa wachezaji ambao wajachoma chanjo hiyo.
Mnamo mwezi disemba, mwaka jana Nets ilibadili uamuzi wake walioutoa awali kuwa nyota huyo asingecheza hadi pale atapopata chanjo ya UVIKO-19 na sasa atacheza msimu uliosalia .
Nyota huyo amecheza mechi yake ya kwanza tangu Juni mwaka jana na sasa amerejea dimbani akiisaidia Nets kushinda mechi yake ya kwanza baada ya vipigo vitatu mfululizo.
Kyrie ni bingwa mara moja wa NBA akiwa na Cleveland na pia amewahi kushinda tuzo ya chipukizi bora wa mwaka wa ligi hiyo mwaka 2012.

