
Max Vesrtappen dereva wa Red Bull kushoto na Charles Leclerc wa Ferrari upande wa kulia
Verstappen pia ni mshindi wa Saudi Arabia Grand Grand Prix wakati Leclerc ni mshindi wa Bahrain na Australiani Grand Prix 2022. Utofauti wa alama umetokana na Max Verstappen kushindwa kumaliza mbio za Bahrain na Australia kwasababu gari lake lilipata itirafu kwenye mfumo wa mafuta kwenye mbio zote mbili.
Msimamo wa Madereva F1 na alama zao.
1. Charles Leclerc alama 86 (Ferrari)
2. Max Verstappen alama 59 (Red Bull)
3. Sergio Perez alama 54 (Red Bull)
4. George Russell alama 49 (Mercedes Benz)
5. Carlos Sainz alama 38 (Ferrari)
Gari ya Charles Leclerc kushoto akichuana na Max Verstappen upande wa kulia
Na Bingwa mara 7 Lewis Hamilton raia wa uingereza dereva wa Mercedes Benz yupo nafasi 7 akiwa na alama 28. Baada yam bio za Wikiendi iliyopita za Emilio Romagna mbio zinazofata za 5 za msimu ni Miami Grand Prix zitakazofanyika Mei 8 2022 nchini Marekani.