
Mshambuliaji wa Bayern Munchen Robert Lewandowski
Lewandowski amekuwa akiongea hadharani kuhusu nia yake ya kutaka kuihama Bayern Munchen majira haya ya joto, na kwasasa anaweka nguvu ya ushawishi kwa timu hiyo kufikiria kumuuza huku klabu ya Barcelona ikiwa ni mahali pekee anapo pendelea zaidi kucheza msimu ujao.
Mwezi uliopita mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliwasilisha ombi la kutaka kuhama na pia hakusita kuishutumu timu yake ya sasa kwa kukosa uaminifu na heshima baada ya miaka minane aliyo hudumu na kuwawezesha kubeba mataji.