Ijumaa , 7th Apr , 2017

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane atakosa michezo ya timu hiyo iliyobaki katika msimu huu kutokana na majeruhi ya goti, aliyoyapata, kwenye mchezo wa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Everton Jumamosi iliyopita.

Sadio Mane

Kwa mujibu ya taarifa ya kocha wa timu ya Liverpool, Jurgen Kloop, Msenegali huyo, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti, na itamchukua muda mrefu kupona.

Mane hadi sasa, ameifungia Liverpool, mabao, 13, tangu ajiunge na majogoo hao wa Anfield, akitokea Southampton majira ya kiangazi mwaka uliopita.