Alhamisi , 3rd Jun , 2021

Mchezaji bora wa Serie A, Romelu Lukaku amesema ataendelea kusalia katika klabu ya Inter Milan msimu ujao, amesema hayo kufuatia tetesi za kuhusisha kuhitajika na vilabu vya England Manchester City na Chelsea.

Romelu Lukaku

Inaaminika baada ya kocha Antonio Conte kuachana na Inter Milan, kuna kundi kubwa la wachezaji litatoka pia kutokana na hali mbaya ya uchumi inayopitia klabu hiyo.

Lukaku amezungumzia Kuhusu hatima yake ndani ya Inter na amesema kuwa bado ataendela kusalia kwenye klabu hiyo,

“Ndio ninabaki, najisikia vizuri Inter. Nimeshawasiliana na mtu ambaye atakuwa kocha wetu mpya, labda sikupaswa kusema hili sasa lakini yalikuwa mazungumzo mazuri. Pia kuna changamoto ya kushinda tena ubingwa”

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubeligiji alitajwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A’ msimu uliomalizika wa 2020-21 baada ya kuisaidia klabu ya Inter Milan kutwaa ubingwa wa Ligi hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11, ambapo alifunga jumla ya mabao 24 na kutoa pasi za usaidizi wa mabao (Assists) 11 akimshinda Cristiano Ronaldo wa Juventus.

Lukaku mwenye umri wa miaka 28 anamkataba na Inter Milan mpaka Juni 30, 2024 lakini amekuwa akihusishwa kuondoka Inter, kutokana na hali mabya ya uchiumi ya klabu hiyo ambapo inawalazimu kuuza baadhi ya wachezaji ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama.

Inaripotiwa kuwa Chelsea na Manchester City ndio timu zinazomuwania kwa ukaribu mshambuliaji huyo, na mmiliki wa Chelsea Roman Abromovic ndio anayetajwa kuwa anamuhitaji mshambuliaji huyo akiwa na imani ataipeleka klabu kule wanakotaka kufika.