Ijumaa , 18th Jan , 2019

Kuelekea mchezo wa pili wa kundi D, Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya AS Vita Club na Simba, mlinda mlango namba moja wa Simba, Aishi Manula amesema amejiwekea malengo mawili ambayo anataka kuyafanikisha.

Aishi Manula (katikati) akishangalia na sehemu ya benchi la ufundi la Simba

Akiongea baada ya mazoezi ya jana usiku kwenye uwanja wa Martyrs zamani ukijulikana kama Kamanyola, Manula amesema atahakikisha anaisaidia klabu yake kuweka historia katika michuano hiyo.

''Vita Club ni timu kubwa Afrika na tunaheshimu uzoefu wake kwenye michuano hii, lakini mimi nitahakikisha kuwa klabu yangu inaweka historia ya kushinda hapa na kisha mimi mwenyewe kutengeneza maisha yangu'', amesema Manula.

Kwa upande wake Jonas Mkude yeye amesifu maandalizi yao na kusema yanaridhisha kuingia katika mchezo mkubwa kama huo hivyo watafanya kile mwalimu alichowaelekeza ili kuweza kupata matokeo mazuri.

Mabao ya Simba kwenye mechi 5 za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

Jumla ya mabao 15
Meddie Kagere 5
Clatous Chama 4
John Bocco 3
Emmanuel Okwi 2
Jonas Mkude 1