
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF imesema sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Namba 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa marudiano wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8 mwaka huu badala ya Mei 7.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kupisha mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho utakaopigwa Mei 7.
Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8 mwaka huu badala ya Mei 7.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga ambapo Mei 7 mwaka huu uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.