Alhamisi , 20th Aug , 2020

Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, Liverpool itaanza harakati ya kutetea taji lake kwa kucheza dhidi ya Leeds United,katika msimu mpya wa EPL ambayo itaanza kutimua vumbi Septemba 12 mwaka huu.

Kiungo wa Manchester City Rodri, akikatiza mbele ya Scott McTominay na Jese Lingard wa Manchester United katika dabi baina ya miamba hiyo miwili ya Jiji la Manchester.

Liverpool itakua mwenyeji wa Leeds ambao watacheza mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu baada ya miaka 16 kupita.

Fulham ambayo imepanda daraja itakabiliana na Arsenal wakati West Bromwich Albion itacheza dhidi ya Leicester City.

Klabu ya Tottenham Hotsurs itakua mwenyeji wa Everton,West ham united itakipiga dhidi ya Newcastle United ,na Crystal Palace itakua mwenyeji wa Southampton.

Chelsea itakua ugenini kucheza dhidi ya Brighton&Hove Albion septemba 14 ,lakini Manchester City na Manchester United hazitocheza michezo yao ya kwanza ili kupata nafasi ya mapumziko kufuatia kuwa na majukumu katika michuano ya Ulaya.

Manchester United ilipaswa kufungua dimba dhidi ya Burnley wakati Manchester City illitakiwa ianze kampeni zake za msimu huu dhidi ya Aston Villa.

Dabi ya jiji la Manchester imepangwa kupigwa Disemba 12 mwaka huu wakati marudiano ni machi 6 mwakani.

Liverpool na Manchester United zitaumana Januari 16 mwakani katika uwanja wa Anfield na zitarudiana mei mosi mwakani katika dimba la Old Trafford.