
Juma Abdul enzi zake akiwa na Klabu ya Yanga
Juma Abdul ambaye aliichezea Yanga kwa mafanikio, amesema ni vyema wachezaji wanaochipukia kuhakikisha wanapoamua kujiunga na vilabu hivyo wahakikishe wanauwezo wa kupigania nafasi ya kucheza.
''Nadhani ni vyema wachezaji wanaohitaji kujiunga na Simba hata Yanga wanapaswa kupigania nafasi ya kucheza mara kwa mara, kivyume na hapo wataishia kutolewa kwa mkopo na biashara yao itaishia hapo'' alisema Juma Abdul.
Beki huyo wa kulia ambaye aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa TPL, kwasasa amejiunga na DTB inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza(Championship) msimu wa 2021/2022.