Jumanne , 8th Dec , 2020

Wawakilishi wa Tanzania Bara katika Kombe la Shirikisho, Namungo Fc wamesonga mbele baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika, CAF kuiondoa timu ya Al Rabita Fc Juba ya Sudan Kusini.

Kikosi cha Namungo Fc ambacho kinaendelea kuiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika.

Awali CAF ilifuta mechi ya marudiano kati ya AL rabita Fc Juba na Namungo Fc iliyokuwa ichezwe Jumapili, Desemba 6 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam baada ya timu hiyo ya Sudan Kusini kushindwa kukamilisha taratibu kuhusu waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi hiyo.

Kutokana na uamuzi huo wa CAF, sasa Namungo Fc imesonga mbele na itacheza raundi ya pili ya mchujo ya Kombe la Shirikisho dhidi ya El Hilal Obeid ya Sudan.

Mechi ya kwanza itachezwa Desemba 23 mwaka huu Azam Complex , Dar es salaam wakati ile ya marudiano itafanyika nchini Sudan ati ya Januari 5 na 6 mwakani.