Jumanne , 4th Jan , 2022

Mchezaji wa Tenisi anayeshikilia nambari kumi na tatu kwenye viwango vya ubora duniani, Naomi Osaka amerejea kwa kishindo kwenye michuano ya kuweka utimamu wa mwili kabla ya kuanza kwa Australian Open.

Bingwa huyo mtetezi wa Australian, alikuwa na alianza taratibu aliporejea uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya miezi minne lakini bado alifuzu kwa raundi ya pili ya mashindano ya Melbourne Summer Set kwa ushindi wa 6-4 3-6 6-3 dhidi ya Alize Cornet asubuhi ya leo Jumanne.

Osaka, ambaye mara ya mwisho alicheza kwe michezo ya ushindani alipofungwa na Leylah Fernandez katika raundi ya tatu ya U.S. Open Septemba mwaka jana, alionyesha kurejea kwa nguvu lakini mara nyingi alikosa usahihi katika michuano hiyo ya kujiandaa kwa Australian Open.

Mjapani huyo anatazamia kurejesha makali yake kwenye michuani ya wazi ya mwaka huu yatakapoanza siku ya Januari 17 mjini Melbourne.