
Akiwa nahodha wa Serbia alikuwa akitazamiwa kuingoza Taifa lake kwenye kundi J, dhidi ya Norway, Chile na Hispania. Miaka miwili iliyopita Serbia waliifunga Hispania kwenye fainali ya ATP cup team.
Hali hii inatia wasi wasi kwa wapenzi wa michezo Tenisi, kuwa nyota huyo atakosa michuano ya wazi ya Australia unaotarajia kuanza mwezi wa kwanza tarehe 17 kwenye mji wa Melbourne.
Sababu kubwa ya Djokovic kujitoa kwenye michuano ya ATP ni kutokana na sheria za Australia kutoruhu wageni kuingia nchini mwao pasipo kupata chanjo ya UVIKO-19, ambayo Djokovic amekataa kuweka wazi kama amechoma au la!