Jumatatu , 12th Feb , 2024

Rais wa Kenya William Ruto ametuma salamu za pole kwa familia ya Mwanariadha Mkenya Kelvin Kiptum aliyefariki kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kaptagat kwenye barabara ya Elgeyo Marakwet-Ravine akiwa anaelekea mjini Elderot Jumapili ya Februari 11-2024

Rais Ruto ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao X kwamba Kelvin Kiptum alikuwa ni miongoni mwa nyota bora duniani aliyevuka vikwazo vingi kwenye mbio za marathoni na kuwa shujaa akiwa na umri wa miaka 24 kupitia mbio kubwa kama Valencia, Chicago na London.

Kiptum amefariki pamoja na kocha wake Mnyarwanda Gervais Hakizimana kwenye ajali hiyo huku nyota huyo aliweka rekodi ya Dunia ya kukimbia kilometa 42 ndani ya Saa 2 na Sekunde 35 kwenye mbio za Chicago Marathon 2023 nchini Marekani huku tayari alikuwa amejumuishwa ndani ya timu ya Kenya itakayoshiriki michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.