Jumanne , 5th Dec , 2023

Taarifa za Kikachero kutoka Afrika Kusini zinaeleza kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika juu ya uhamisho wa Ranga Chivaviro kutoka Kaizer Chiefs kwenda Young Africans.

Wakala wa Ranga Chivaviro, Herve Tra Bi, amesema kuwa “Ranga haendi popote kwa sasa. Ana mkataba wa miaka miwili na Kaizer Chiefs. Tunahitaji kuheshimu mkataba wake na Chiefs,” .

Hii ni baada ya tetesi kadhaa kuvuma zikidai kwamba Ranga tayari amekamilisha usajili wa mkopo kujiunga na Wananchi januari 2024.