Ijumaa , 20th Mei , 2016

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta, usiku wa kuamkia hii leo ameisaidia timu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa mchujo wa sita bora ya Ligi Kuu ya Ubelgiji kuwania kucheza michuano ya Ulaya.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta akiwajibika uko nchini Ubelgiji.

Samatta alicheza kwa dakika zote 90, mabao ya Genk yakifungwa na Leon Bailey dakika ya 45, Buffel dakika ya 65, Pozuelo dakika ya 76, Ndidi dakika ya 78 na Nikos Karelis dakika ya 90 na ushei wakati ya Anderlecht yalifungwa Filip Djuricic dakika ya 25 na Suarez dakika ya 60.

Genk sasa itahitaji ushinda katika mchezo wao wa mwisho Jumapili dhidi ya Genk ugenini ili kufuzu moja kwa moja Europa League.

Club Brugge inaongoza mchujo wa kuwania michuano ya Ulaya kwa pointi zake 53, ikifuatiwa na Anderlecht yenye pointi 44, AA Gent pointi 41 na Racing Genk pointi 39.

Timu itakayomaliza katika nafasi ya nne, ili kupata tiketi ya kucheza Europa League italazimika kumenyana na mshindi kati ya Charleroi na Kortrijk zitakazomenyana katika mchezo mwingine wa mchujo.

Samatta jana amecheza mechi ya 15 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza ndandi barani Afrika.

Katike mechi hizo, ambazo nane tu ndiyo ameanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao nne, moja katika kila mechi Genk ikishindia 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem, 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.