
Mbwana Samatta katika mchezo dhidi ya AFC Bournemouth
Katika mchezo huo ambao Aston Villa ilikuwa ugenini, Samatta alifunga bao moja licha ya timu yake kufungwa mabao 2-1.
Akihojiwa na mtandao wa klabu, Samatta amesema kuwa wao kama wachezaji wamejisikia vibaya kupoteza mchezo huo hasa katika kipindi hiki cha mwisho wa msimu, pamoja na bao alilofunga.
"Tumesikitishwa kama kundi, hatukupata kile tulichokihitaji. Wakati wote ukipoteza mchezo kunakuwa na wakati mgumu", amesema Samatta.
"Sijayazoea vizuri mazingira ya Uingereza, nitazoea haraka kwa sababu ninatokea ligi ya Ubelgiji, japo ushindani hapa ni mkubwa kwahiyo inanibidi nielewe kila kitu na nikishaelewa kila kitu nitakuwa na wakati mzuri zaidi wa kuisaidia timu", ameongeza.
Aston Villa ipo katika nafasi moja juu (17) ya mstari wa kushuka daraja, ikiwa na pointi 25 baada ya kushuka dimbani michezo 25.