Tetesi za kukamilika kwa usajili huo zimezidi kusambaa mchana huu baada ya kubainika nyota huyo raia wa Chile hajasafiri na kikosi cha Arsenal kilichosafiri leo kwenda kuivaa Bournemouth kwenye mchezo wa EPL.
Ripoti mbalimbali kutoka nchini England zinaeleza kuwa Sanchez mwenye umri wa miaka 29, ameachwa kwa ajili ya kukamilisha masuala yake ya usajili huku klabu ya Manchester United ikitajwa kuwa kinara katika mbio hizo.
Mkataba wa Sanchez na Arsenal aliyesajiliwa mwaka 2014 akitokea Barcelona unamalizika mwezi Juni na endapo Arsenal haitamuuza katika kipindi hiki cha dirisha dogo ataondoka bure ifikapo mwezi Juni.
Makocha wawili wenye ushindani mkubwa Pep Guardiola wa Man City na Jose Mourinho wa Man United wapo kwenye kinyang'anyiro cha kumwania mchezaji huyo ambaye msimu huu amefunga mabao saba kwenye EPL.
