Shirikisho lavunja kambi ya timu ya taifa

Jumapili , 8th Sep , 2019

Wakati Taifa Stars ikishuka dumbani leo dhidi ya Burundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2022, kwa upande wa Afrika Kusini mambo sio mazuri.

Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini (SAFA), limevunja kambi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo baada ya kukosa mechi za kujipima nguvu.

SAFA ilituma maombi kwa nchi zaidi ya tano za Afrika, zikiwemo Zambia na Madagascar, kuomba kucheza nazo, ambapo awali zilikubali kabla ya baadaye kukataa.

Imeelezwa sababu ya nchi hizo kukataa ni kutokana na kukasirishwa na vitendo vya vurugu zinazoendelea nchini humo.

Wikiendi hii baadhi ya mataifa yanacheza mechi za awali kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambapo ukiacha Tanzania mechi nyingine ni,

Lesotho dhidi ya Ethiopia, Equatorial Guinea dhidi ya Sudan Kusini na Siera Leone dhidi ya Liberia.