Wachezaji wa Simba wakishangilia goli
Simba itashuka Dimbani leo Usiku Saa2:15 kwenye mchezo wa kundi B, na kuelekea mchezo huo kocha wa kikosi hicho Pablo Franko amesema
“Hatukupata muda wa kujiandaa lakini tunapaswa kushinda kila mchezo. Tutafanya mabadiliko kidogo ya kikosi kwa ajili ya kuwalinda wachezaji. Tumeongeza wachezaji wengine kwa ajili ya majaribio ambao tutawatumia katika mashindano haya na wakituvutia tutawapendekeza kwa uongozi wasajiliwe.” amesema Pablo.
Tayari kikosi cha Simba kimefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya mapinduzi. Lakini mchezo wa mapema leo unachezwa Saa 10:15 Jioni Yanga SC watacheza dhidi ya KMKM, michezo yote hii inachezwa katika dimba la Amaani

