Simba wathibitisha kuondoka kwa Patrick Aussems

Jumanne , 19th Nov , 2019

Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kuwa kocha wake mkuu, Patrick Aussems hayupo nchini kwa dharura.

Kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems

Mtendaji mkuu wa Simba Senzo Mazingiza amethibitisha kuondoka kwa kocha huyo huku akishindwa kuweka wazi kuwa ni lini atarejea.

'Ni kweli ameondoka kwa dharura, kuhusu alipo na atarejea lini siwezi kueleza sana ila email yake ya mwisho alisema atarudi Jumatano', amesema Senzo.

Simba ilicheza mchezo wa kirafiki hivi karibuni na kufungwa goli 2-1 na KMC.