Ijumaa , 9th Mei , 2014

Klabu ya Simba imesema kuwa bado iko katika mikakati ya kuanza zoezi la usajili kimya kimya kwa kuzingatia mahitaji muhimu ya timu hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya Usajili Simba SC

Kamati ya usajili ya klabu ya soka ya Simba imesema kuwa bado iko katika mikakati ya kuanza zoezi la usajili kimya kimya huku wakizingatia mahitaji muhimu ya timu hiyo kwa mujibu wa ripoti ya kocha mkuu wa timu hiyo mcroatia Zdravko Logarusic.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hans Pope amesema wakati wowote kuanzia sasa kamati yake itakutana na kamati ya utendaji ya timu hiyo tayari kujipanga na kuanza kufanyia kazi ripoti ya mwalimu Logarusic

Aidha amesema pamoja na baadhi ya vilabu kuanza usajili wao mapema watafanya kisayansi zadi kutokana na mahitaji ya timu na kwa kufuata utaratibu.