
Baada ya kuwasili wachezaji wamepewa mapumziko ya kwenda kukutana na familia zao na kesho wataanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Ijumaa, Desemba 30.
Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema lengo letu lilikuwa kuchukua pointi zote tisa za Kanda ya Ziwa kwenye mechi tatu lakini tumefanikiwa kupata saba.
“Kikosi kimerejea salama Dar es Salaam na wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja na kesho tutarudi mazoezini kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons,” amesema Rweyemamu.
Katika mechi tatu za Kanda ya Ziwa tumeshinda mbili dhidi ya Geita (5-0), KMC (3-1) na sare ya bao moja na Kagera Sugar.