Jumatano , 28th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Simba imetangaza kuwa leo itakamilisha usajili wa beki wa kimataifa kutoka Ivory Coast kwaajili ya kuziba pengo la mlinzi wa pembeni wa kulia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi.

Zana Coulibaly

Kwa mujibu wa taarifa ya Simba mlinzi huyo ni Zana Coulibaly kutoka klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast na taaratibu za awali tayari zimeshafanyika.

''Tunapenda kuwatangazia kwamba beki Zana Coulibaly kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast leo anawasili nchini kwa ajili kukamilisha taratibu za usajili'', imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa usajili huo ni kuziba pengo la beki Shomari Kapombe ambaye siku za karibuni alipata majeraha katika kambi ya timu ya taifa 'Taifa Stars' ilipokuwa ikifanya maandalizi ya mwisho dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho .

Katika mchezo huo wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Lesotho uliopigwa Novemba 18, Stars ilipoteza kwa bao 1-0. Ikumbukwe kuwa Simba inashuka dimbani hii leo dhidi ya Mbabane Swallows katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam saa 10 jioni.