Jumapili , 2nd Jul , 2017

Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Simba imemteua Salim Abdallah na Iddy Kajuna ambao ni wajumbe wa kamati hiyo, kuwa wasimamizi wa majukumu ya Rais Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange kutokana na viongozi hao kushikiliwa na vyombo vya dola.

Hayo yamebainishwa na Kamati hiyo iliyokutana jana Jumamosi katika kikao cha dharura, baada ya viongozi wake wa ngazi za juu kukosa dhamana kwenye kesi yao iliyokuwa ikiendeshwa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, juu ya makosa yao yanayowakabiri ya kutakatisha fedha kinyume cha sheria.
Ujumbe mwenyewe kutoka kwa kamati ya Simba.