
Samatta akikabidhiwa jezi tayari kuitumikia Klabu yake Mpya ya Genk ya nchini Ubelgiji
Samatta amesema, alikuwa na furaha iliyopitiliza kwani kwake ni ndoto ya siku nyingi na alikuwa anatamani itimie haraka na imekuwa kweli.
Samatta amesema, anaiheshimu TP Mazembe, anamuheshimu Rais wa Mazembe Moise Katumbi hawezi kuwa na matatizo yoyote kwasababu walimchukua tangu akiwa mdogo na kumlea na amekulia katika klabu hiyo akisubiri wakati muafaka hadi klabu yake ifikie makubaliano na klabu iliyomuhitaji.
Samatta amesaini kandarasi ya miaka minne (4) kukitumikia kikosi cha Genk ambapo anatarajia kuhudumu kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2020.