Jumatano , 20th Apr , 2022

Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen amesema anahitaji michezo miwili ya kirafiki kabla ya kuanza kwa michezo ya kufuzu kwenye michuano ya Afcon 2023 inayotarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast

(Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen)

Kocha Poulsen amesema lengo la Stars ni kufuzu kwenye michuano hiyo licha ya kutowafahamu vyema wapinzani kama Niger lakini ana matumaini makubwa kwa Stars kufuzu kwenye michuano hiyo.

Tunahitaji kupata michezo miwili ya kirafiki ili tuwe na mwanzo mzuri kabla ya kuanza harakati za kufuzu ,utofauti mkubwa wa michuano hii na ile ya kufuzu kombe la dunia ni kwamba kule ni timu moja tu inafuzu ila michuano hii kuna nafasi mbili za kufuzu na kutupa nafasi kama sisi tuliokwenye nafasi za chini ya viwango vya FIFA kuwa na matumaini makubwa ya kufuzu na lengo letu ni kufuzu kwenye michuano hiyo”amesema Kim Poulsen

Tanzania imepangwa kundi F sambamba na mabingwa wa Afcon 2019 Algeria ,Uganda na Niger kusaka tiketi ya kwenda kushiriki kwenye makala hayo ya 34 tangu yaanzishwe huku mara ya mwisho kwa Stars kushiriki kwenye fainali hizo ilikuwa mwaka 2019 nchini Misri.