TFF yatoa onyo kali kwa matapeli kuelekea AFCON

Jumatano , 15th Mei , 2019

Shirikisho la soka Tanzania TFF, limepiga marufuku kwa watu wote wanaotumia vibaya nembo ya shirikisho hilo kutangaza gharama za usafiri pamoja na hoteli kwa Watanzania watakaokwenda nchini kwenye fainali za AFCON.

Makao Makuu ya TFF

TFF imewataka watu hao kuacha kusambaza vipeperushi vyenye nembo ya shirikisho, ikiita kitendo hicho kuwa ni matumizi mabaya ya nembo ya taasisi.

Taarifa hiyo imesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika kutumia nembo ya shirikisho katika shughuli hiyo.

Taarifa nzima ya TFF kuhusiana na onyo hilo hii hapa chini.