Timu ya Ligi kuu yaenda nje kujiandaa na mechi

Jumanne , 8th Oct , 2019

Timu ya soka ya Alliance FC inayocheza ligi kuu soka Tanzania bara, imeondoka leo jijini Mwanza kuelekea nchini Kenya, tayari kwa maandalizi ya michezo yetu ijayo ya VPL.

Alliance FC

Uongozi wa Alliance umeeleza kuwa timu inakwenda nchini Kenya kwa mwaliko wa timu ya GMFC, na wenyeji wao hao watawatafutia michezo mingine ya kirafiki wakiwa nchini humo.

Kwa upande wa ligi kuu, Alliance FC inakabiliwa na michezo ya karibuni dhidi ya Yanga SC Ruvu Shooting Tanzania Prisons na Mbeya City.

Kati ya michezo hiyo, mchezo wa dhidi ya Yanga SC pekee ndio utachezwa katika uwanja wa CCM Kirumba, huku michezo mingine yote ikichezwa katika uwanja wa Nyamagana.

Ligi kuu kwasasa ipo mapumziko kupisha ratiba ya kalenda ya FIFA, ambapo timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), itacheza na Rwanda jijini Kigali Oktoba 14.