
Wachezaji wa Warriors na Raptors.
Kwenye game ya kwanza katika series ya best of 7 ya fainal ya NBA, Toronto wamefanikiwa kushinda nyumbani kwa pointi 118 dhidi ya 109 za Warriors.
Toronto walifanikiwa sana kwenye 'defence' ya 'ku-switch' inapotokea 'pick', pia waliweza kupunguza 'score' za mtu kama Kay Thompson akiwa amefunga point 21 hvyo kufanya Warriors kuwa na watu watatu kwenye 'first five' wenye 'double figures' katika pointi.
Wakati Pascal Siakam wa Raptors akifunga pointi 32 na 'first five' ya Raptors ikiwa na wachezaji wanne wenye 'double figures' katika scores.
Series itaendelea tena game two siku ya Jumapili usiku itakayopigwa katika uwanja wa Scotiabank mjini Canada.