Jumanne , 1st Mar , 2016

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Annastazia Wambura amewataka wachezaji wa Twiga Stars kuendeleza nidhamu waliyonayo katika mazoezi ili kujiwekea nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Annastazia amesema, Wizara yake itahakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwa kutatua changamoto zilizopo katika timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wachezaji ili kuzidisha juhudi katika mashindano.

Mh. Wambura amesema, Wizara yake imeweza kupata fedha kwa ajili ya Twiga Stars ambazo zitagawanywa kwa wachezaji iwapo wataweza kufanya vizuri katika mchezo wa awali dhidi ya Zimbabwe.

Amesema katika fedha hizo kila mchezaji atapata shilingi laki tatu na pia wakifanikiwa kuifunga tena katika mchezo wa marudiano pia watapewa laki tatu na iwapo hawatafanikiwa kuifunga timu hiyo basi pesa hizo zitakabidhiwa kwa Uongozi wa timu ili ziweze kutumika katika mahitaji yaliyopo.