Jumanne , 22nd Sep , 2020

Michezo ya raundi ya tatu ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2020-21 ilikamilika jana kwa kwa michezo miwili na kukamilisha idadi ya michezo 27 katika roundi zote tatu zilizochezwa mpka sasa.

Mshambuliaji wa Simba SC Meddie Kagere amemaliza kinara wa ufungaji wa ligi kuu tTanzania bara kwa misimu miwili mfululizo akifunga jumla ya mabao 45

Kwenye michezo 9 ya raundi ya tatu tumeshudia yakifungwa mabao 14 ambao ni wastani wa bao 1.5 kwa kila mchezo. 

Katika michezo ya roundi ya tatu ni timu mbili tu katika roundi hii ya ambazo zimefanikiwa kufunga mabao kuanzia mawili ni Simba ambayo ilikfunga mabao 4 kwenye ushindi walioupata wa mabao 4- 0 dhidi ya Biashara United na KMC ambayao ilishinda mabao 2 – 1 dhidi ya Mwadui FC.

Ukichukua michezo yote 27 iliyochezwa mpaka sasa katika roundi zote tatu yamefungwa jumla ya mabao 41 ambao ni wastani wa bao 1.518 kwa mchezo.

Wastani wa bao 1 kwa mchezo ni wastani mdogo sana na unatengeneza maswali mengi juu ya ubora wa washambuliaji wetu.

Katika michezo yote 27 iliyochezwa mpaka sasa ni timu mbili tu ndizo zilizofanikiwa kufunga zaidi ya mabao mawili kwenye mchezo mmoja. 

Ni KMC ambao walipata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Mbeya City na klabu ya Simba ambayo iliifunnga Biashara United mabao 4-0 ndizo timu pekee ambazo zimefanikiwa kufunnga zaidi ya mabao mawili kwenye mchezo mmoja.

Ukijaribu kufunanisha na ligi inayoshabikiwa na kupendwa na watu wengi Duniani ligi kuu ya England EPL, ligi hiyo imezalisha jumla ya mabao 44 katika michezo yake ya raundi ya pili peke ya katika michezo 10 ukiwa ni wastani wa magoli 4.4 yamefungwa kwa kila mchezo katika michezo ya raundi ya pili ya ligi hiyo. 

Labda tujiulize inawezekana timu zetu zinasafu bora za ulinzi ndio maana tunashuhudia yakifungwa mabao machache au washambuliaji wetu ni butu uwezo wao wa kufunga ni mdogo?

Ukitazama michezo mingi ya ligi kuu bara VPL timu zetu zinatengeneza nafasi chache sana za kufunnga na hata hizo nafasi zimekuwa hazitumiwi vizuri.

Upotezaji wa nafasi za wazi umekuwa mkubwa  kwa wachezaji wanao cheza katika safu ya ushambulliaji pia hakuna ubunifu katika kutengeneza nafasi za mabao kutoka katika idara ya kiungo.

Hivyo inawezekana tunashuhudia uhaba huu wa mabao kwa sababu ligi yetu haina wachezaji wa daraja la juu katika safu za ushambuliaji katika vilabu vyetu, ingawa wapo wachache ambao wameonyesha ubora wao kupachika mabao .
Mfano washambuliaji wa Simba SC Meddie Kagere, na John Bocco, na mshambuliaji wa Azam FC  Obrey Chirwa hawa wamejipambanua kutokana na muendelezo bora walionao mbele ya goli.

Ifuatayo ni orodha ya wachezaji wanaoongoza kwa kufunga mabao mpaka sasa katika msimu huu mpya wa 2020-21 wa VPL ambapo wamefungana wachezaji watano wachezaji hao ni .
.
1. Clatous Chama-Simba SC mabao 2
2. Mzamiru Yassin -Simba SC mabao 2
3. Prince Dube -Azam FC mabao 2
4. Reliants Lusajo -KMC FC mabao 2
5. Hassan Kabunda- KMC mabao  2