Alhamisi , 26th Dec , 2019

Baada ya mechi ya Tanzania Prison dhidi ya Yanga kubadilishwa uwanja kutoka CCM Sokoine Mbeya na kupelekwa Samora Iringa, wapinzani wao Simba wameendelea kujivunia takwimu za kocha wao mpya.

Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck

Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, Simba wameweka takwimu za matokeo ya mechi mbili alizofundisha kocha wao mpya Sven Vandenbroeck.

Katika mechi hizo mbili Simba imeshinda zote na kufunga jumla ya magoli 10 huku ikiwa haijaruhusu kufungwa goli. 

Simba imeshinda goli 6-0 dhidi ya Arusha FC kwenye kombe la shirikisho na ikashinda 4-0 dhidi ya Lipuli FC kwenye mchezo wa ligi kuu siku ya jana Disemba 25, 2019.

Yanga na Tanzania Prison zitacheza kesho kwenye uwanja wa Samora Iringa. Mbali na hilo uwanja wa Sokoine umefungiwa na Bodi ya ligi kutumika katika mechi za ligi kuu, ligi darala la pili na ligi daraja la kwanza.