Waliopitishwa kugombea Uenyekiti Yanga

Jumanne , 9th Apr , 2019

Kamati za Uchaguzi za klabu ya Yanga pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania TFF zimekutana leo kufanya mchujo wa wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya klabu hiyo.

Makao Makuu ya Yanga

Kikao hicho kimewapitisha wagombea wote lakini kamati zimewapa angalizo kuhakikisha wanakamilisha nyaraka ambazo zimekosekana katika fomu zao, ambazo wametakiwa kufika nazo siku ya usaili.

Majina yaliyopitishwa kugombea nafasi ya Uenyekiti Yanga ni Dkt. Mabette Mshindo Msola, Lucas Mashauri na Elias Mwanjala huku katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, majina yaliyopitishwa ni Janeth Zebedayo Mbena, Fredrik Wilfred Mwakalebela, Thobias Lingalangala na Samwel Lukumay.

Waliopitishwa kugombea Yanga

 

Wagombea hao waliopitishwa wataungana na wale waliopitishwa katika mchakato wa awali wa uchaguzi ulioendeshwa na TFF, ambao uliwapitisha baadhi ya wagombea akiwemo Dkt. Konas Toboroha katika nafasi ya Uenyekiti.

Kuona majina yote ya wagombea katika uchaguzi unaotarajia kufanyika mapema mwezi ujao, tazama taarifa hapa chini.