
Musa Mgosi
Mgosi ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya vijana ya Simba, amesema kuwa Azam FC inatakiwa kujitathmini namna ya kutumia vizuri wachezaji wao kwa mashindano mbalimbali kwani imekuwa ikitumia wachezaji wao wote wa kikosi cha kwanza.
"Kiukweli mchezo wa fainali ulikuwa ni hamsini kwa hamsini, lakini Azam FC ndio ambao wanatakiwa wajiangalie zaidi kwasababu wamechezesha kikosi chao chote ambacho kinaaminika kitawapa ubingwa wa Ligi Kuu lakini wamepata upinzani mkubwa kutoka kwa Simba ambayo ilikuwa na wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza", amesema Mgosi.
"Wanapaswa wajitazame zaidi kuwa wanatakiwa wafanye nini ili waweze kuhimili vishindo kama hivyo na kuweza kufanya vizuri", ameongeza.
Pia Mgosi amezungumzia utaratibu wa klabu hiyo wa kupandisha wachezaji kutoka timu za vijana, akisema kuwa huo ni utaratibu wa klabu hiyo kuwa kila msimu ni lazima ipandishe wachezaji kwenda kikosi cha kwanza.