Jumanne , 4th Oct , 2022

Kikosi cha Al Hilal kutua Jijini Dar es Salaam Alhamisi wakitokea nchini Congo,tayari kwa kuikabili Yanga kwenye mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Afrika utakaopigwa jumamosi tarehe 8 mwenzi huu.

Al Hilal

Hilal kwa sasa bado ipo DR Congo ikiendelea kujiweka fiti ambapo kwenye ziara yao hiyo nchini humo tayari wameshacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Don Bosco siku ya Jumapili na kushushiwa kipigo cha mabao 3-1, ambapo wachezaji wa Don Bosco walivaa jezi za TP Mazembe katika mchezo huo.

Hata hivyo kikosi hicho leo asubuhi kimeendelea kujifua kikiwa chini ya kocha mkuu Florient Ibenge.

Ikumbukwe mabingwa hao wa Sudan walisonga mbele na kuingia kwenye hatua hii baada ya kuitoa St. George ya Ethiopia kwa bao la ugenini ambapo kwenye mchezo wa kwanza wakiwa ugenini walifungwa mabao 2-1 kisha waliporudi nyumbani wakaibuka na ushindi wa bao 1-0