Jumatano , 20th Apr , 2022

Wachezaji wa Tennis wa nchi za Urusi na Belarus watakutana na rungu la kupigwa marufuku kushiri Mashindano ya Ubingwa ya wimbledon kutokana na uvamizi wa kivita nchini Ukraine.

(Mchezaji wa Tennis namba 2 kwa ubora duniani Raia wa Urusi Daniil Medvedev)

Wimbledon imeonyesha kuwa tayari kuthibitisha kufungiwa kwa wachezaji wote kutoka nchi za Urusi na Belarus kutoshiriki Mashindano ya msimu huu wa majira ya joto kutokana na ukatili wa kivita unaoendelea nchini Ukraine, ambako matumaini ya mazungumzo ya amani yanaonekana kufifia.

Kamati kuu ya vilabu vyote vya mchezo wa Tennis vya England inaonekana kufikia uamuzi wa kuchua hatua hiyo kwa haraka zaidi kabla ya mkutano na waandishi wa habari wa kila mwaka uliopangwa kufanyika wiki ijayo, ambapo taarifa hiyo ndio lilipaswa kutolewa.

(Mcheza Tennis namba 4 kwa wanawake duniani Aryna Sabalenka wa Belarus)

Ziara za WTA na ATP zimearifiwa kwamba wachezaji wake bora watapigwa marufuku kushiriki katika mashindano ya SW19 na taarifa zinasema uamuzi huo uko karibu kupitishwa, huku mchezaji nambari 2 kwa ubora duniani kwa upande wa wanaume Daniil Medvedev na mchezaji nambari 4 kwa ubora duniani upande wa wananwake Aryna Sabalenka wakiwa miongoni mwa nyota watano (5) kati ya 40 bora wa mchezo huo watakaofungiwa, lakini Medvedev atakua ndiye mchezaji wa hadhi ya juu zaidi kuathiriwa na maamuzi hayo.

Vyombo mbalimbali vya hahari vya kimataifa vimearifu kwamba Urusi na Belarus zitazuiwa na kusimamishwa, Ingawa siku zote ilikuwa inafahamika kuwepo kwa uwezekano wa kufungiwa nchi yoyote itakayokuwa na uvunjivu wa amani.

Wimbledon imefanya maamuzi haya mapema kabla ya tarehe yake ya kuanza mashindano ya Juni 27 na ikiwa ni mapema zaidi kuliko ilivyotarajiwa, kuzingatia misukosuko iliyotokea kabla ya michuano ya Australian Open mwaka huu, ambayo ilijaribu kurekebisha sheria juu ya wachezaji ambao hawaja chanjwa chanjo ya Covid-19 kutoruhusiwa kucheza kama kilichotokea kwa Novak Djokovic kuondolewa mashindanoni.