Ijumaa , 26th Mar , 2021

Xabi Alonso ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya vijana ya Real Sociedad ya Hispania mpaka mwaka 2022 na kufuta uvumi wa kujiunga na klabu ya Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.

Xabi Alonso

Ripoti kutoka nchini Ujerumani ziliripoti kuwa kiungo huyo wa zamani wa Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich atajiunga na Monchengladbach, lakini hii leo imethibitishwa kuwa amefikia makubaliano na Real Sociedad timu yake ya utoto na kasaini mkataba huo.

Matamanio yakutaka kuwa karibu na familia yake lakini kuvutiwa na mpango wa kukuza vijana ndani ya klabu hiyo ndio vitu vilivyomfanya kocha huyo mwenye umri wa miaka 39 kuendelea kusalia klabuni hapo.

Alanso ambaye ni mshindi wa kombe la Dunia akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Hispania mwaka 2010, alimalizia soka lake nchini Ujerumani katika klabu ya Bayern Munich, iliaminika angechukua mikoba ya kocha Marco Rose mwishoni mwa msimu ndani ya klabu ya Borussia Monchengladbach, kuijua na kuizungumza lugha ya kijerumani kulimpa nafasi kubwa zaidi ya kutwaa kibarua hicho, lakini pia amekuwa akaitajwa kuwa huenda siku za mbeleni atakuja kukinoa kikosi cha Liverpool ya England.