Jumanne , 25th Jan , 2022

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amefungukia kuhusu sakata la beki wao Djuma Shaban kuonekana akimpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania Yahya Mbegu baada ya mchezaji huyo kumkanyaga Djuma kwenye mchezo wa NBC Tanzania uliochezwa Jumapili ya Januari 23, 2022 Jijini Arusha,

(kutoka kushoto:Msemaji wa Yanga, Haji Manara na Djuma Shabani)

Manara amesema kuwa kitendo alichokifanya Djuma wa Yanga SC sio kizuri na wenyewe wanakikemea.“Yes sio kitendo kizuri na Yanga tunakikemea hata kama kulikuwa na provocations,(hasira)”.

Baada ya kitendo hicho Djuma hakuchukuliwa hatua yeyote na mwamuzi wa kati wa mchezo huo, Hans mabena kwa kile kinachoelezwa kuwa hakuona tukio hilo. Djuma alifanyiwa mabadiliko kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa uliochezwa kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 35, utofauti wa alama 10 na watani wao wa jadi Simba wenye alama 25 baada ya Yanga SC kucheza mechi 13 za ligi bila kupoteza mchezo hata mmoja.