Jumapili , 16th Jan , 2022

Klabu ya Yanga imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union, na sasa kikosi hicho cha timu ya wananchi kinaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 8. Huu ni ushindi wa kwanza kwa Yanga mkoani Tanga baada ya miaka 6.

Saidi Ntibazonkiza akishangilia baada ya kufunga bao la pili

Mabao ya Yanga kwenye ushindi huo wa mabao mawili yamefungwa na Fiston Mayele aliyefunga bao la kwanza dakika ya 41 na bao la pili limefungwa na Saidi Ntibazonkiza dakika ya 90. Kwa ushindi huu Yanga inafikisha alama 32.

Huu ni ushindi wa 5 ugenini kwa Yanga msimu huu wa 2021-22 katika michezo 7 waliocheza ugenini wakiwa wametoka sare michezo 2, wamevuna alama 17 katika michezo hiyo ya ugenini, lakini pia Yanga wameshinda kwa mara ya kwanza katika dimba la Mkwakwani tangu mwaka 2015 ambapo walishinda bao 1-0.

Yanga wanasalia kileleni mwa msimamo na sasa wanaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 8 dhidi ya Simba wenye alama 24 wakiwa nafasi ya pili lakini Simba wamecheza michezo 10 huku yanga wameshacheza michezo 12.

Mchezo mwingine wa Ligi leo umechezwa huko mkaoni Rulwa ambapo Tanzania Prisons waliwa wenyeji wa KMC FC na mchezo huo umemalizika kwa KMC kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mabao ya Kelvin Kijiri na Ally Ramadhani.