Alhamisi , 5th Mei , 2016

Wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani Jijini Mwanza wameanzisha vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kukabiliana na tatizo la ajira.

Baadhi ya wahitimu bora wa vyuo vikuu mbalimbali wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.

Akizungumza na viongozi wa vikundi hivyo wakati wa uwasilshaji wa Andiko Mradi Mkurugenzi wa Kampuni ya Ubunifu na Uvumbuzi, Aloyce Megelo, amesema vikundi hivyo vimeanzishwa kwa mtaji mdogo kwa ubia na wawekezaji wa ndani.

Amesema kupitia kampuni ya Wananchi ya Bega kwa Bega ambayo wameiwezesha ndio itatumika katika kuzifadhili kampuni hizo zitakazoanzishwa na wajasiliamali hao wadogo ambao ni wahitimu wa elimu ya katika vyuo mbalimbali.

Wakizungumza katika mkutano huo vijana hao wamesema miradi waliyoianzisha mingi inajuhusisha na biashara mbalimbali ambazo zimeonekana ni fursa katika mkoa huo ikiwa ni, Ufugaji na Uuzaji Samaki pamoja na Usindikaji Maziwa.

Nao baadhi ya wawekezaji kutoka Kata ya Kiseke mkoani humo wameunga mkono miradi hiyo iliyoandikwa na wahitimu hao huku wakisema kuwa Wajasiriamali wadogo wanaweza kuwa chanzo kikuu cha kuinua uchumi wa nchi.