
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha Dr Besigye akila kiapo mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya jaji wa mahakama ya juu.
Usalama umeimarishwa nchini humo huku mitandao ya kijamii ikizimwa kwa sababu za kiusalama huku viongozi wengi wakitarajiwa kuhudhuria wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Magufuli.
Wakati hayo yakiendelea sherehe za kumuapisha Rais Yoweri Museveni kushika madaraka kwa awamu ya tano mfulilizo zinaendelea katika uwanja Kalolo.