
Mfano wa namna ambavyo mabweni katika sekondari Namaskata wilayani Tunduru wanavyolala kwenye magodoro chini. (Maktaba)
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Benelith Mahenge kukagua ufanisi wa shughuli za maendeleo katika wilaya ya Tunduru ndipo akaamua kukatisha safari yake pamoja na msafara wake na kutinga katika shule ya sekondari Namaskata na kukuta hali isiyoridhisha ya utoaji malazi kwa wanafunzi .
“Tangu shule ianze kupokea wanafunzi wa kulala mwaka 2009 hadi leo mmekaa tuu kimya na wanafunzi wanateseka, ina maana bila mimi kupita huku hali hii isingeshughulikiwa, jambo hili si jema hata kidogo” Amesema Mahenge
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza hatua za haraka zichukuliwe na watendaji wliopo chini yake katika kuhakikisha wanafunzi wa shule hiyo wanapata vitanda vya kulalia.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Honera amemuagiza afisa elimu wa wilaya hiyo kufanya ukaguzi katika shule zote ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo katika shule zote ili serikali iweze kutimiza wajibu wake.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wamesema wamekuwa wakipatwa na magonjwa ya kuumwa mbavu na migongo kutokana na kulala chini jambo linalofifisha jitihada zao katika kusaka elimu.