Jumapili , 16th Oct , 2016

Serikali imetoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na baadhi ya watu ambao ni matapeli hasa wale wanaotumia njia ya simu.

ACP Advera Bulimba

Tahadhari hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Bulimba wakati akizungumza na East Africa Radio, na kuongeza kuwa wamepokea ripoti nyingi kutoka kwa baadhi ya watu ambao wametapeliwa.

Amesema matapeli hao kila siku wanabuni njia mpya za kutapeli na tayari Jeshi la Polisi limeweka mitego ya kuwabaini matapeli hao kama ilivyowakamata matapeli wengine ambao walikuwa wanapanga kutapeli lakini Jeshi hilo liliwawahi na kuzuia utapeli usifanyike na tayari wako katika vyombo vya dola kwa uchunguzi zaidi.

Amesema wananchi watoe ushirikiano katika kuwafichua matapeli kwani kama hawatawafichua wanaweza wakafanya uhalifu mkubwa zaidi.