
Nay wa Mitego
Akizungumza na www.eatv.tv amesema kwamba kwa kuwa hafikirii sana kufanya kampeni ikitokea akafanya hivyo basi atafanya kampeni kwa wanasiasa wote anaowakubali bila kujali chama.
"Sitaangalia Chama, nitafanya kampeni kwa mgombea ambaye mimi ninamkubali, haijalishi kwamba atakuwa ni wa ACT, CHADEMA au CCM kote nitapita na kupiga kampeni na sivyo kama ambavyo alifanya katika uchaguzi mjuu 2015", amesema.
Mwaka 2015, Rapa Nay wa Mitego alipanda katika majukwa ya UKAWA muungano uliounganisha vyama vya CUF, CHADEMA, NCCR Mageuzi, na NLD.