Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita
Meya Mwita ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, ambapo ameeleza kuwa, kwa sasa amesema wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, kura za wajumbe hazikutosha na kumfanya yeye kuendelea kukaa ofisini.
Meya Mwita amesema kuwa "mimi silazimishi kukaa ofisini kama wanataka kunitoa mimi wafuate taratibu, haiwezekani watu wafoji kura baada ya kuwa na kura 17 wakasahau mmoja yuko nje ya nchi" amesema Meya wa DSM.
"Nilisema jana viongozi wa dini walifanya kazi waliniombea sana, tena nimeshangaa sana hawa watu wamefoji mchana kweupe, tena wala hawajakamatwa" ameongeza Mwita.
Tazama video kamili hapo chini.