Jumatatu , 27th Apr , 2020

Wakati  Serikali ikiendelea kuhamasisha wananchi kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, matumizi ya viungo vya liomao, tangawizi na vitunguu saumu, yameonekana kushika kasi katika maeneo mbalimbali jijini Arusha kwa kile kinachoaminika, vitu hivyo husaidia kuimarisha kinga ya mwil

Wauzaji wa malimao, vitunguu saumu na tangawizi Arusha

Achilia mbali na biashara hiyo kuonekana lulu sokoni, lakini kwa sasa imeonekana kuwa maarufu mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, ambapo baadhi ya vijana wanaojishughulisha na biashara hii wanasema kwao ni fursa, kutokana na uhitaji wa bidhaa hiyo kwa sasa kuwa maradufu ukilinganisha na hapo awali.

"Tumeamua kujitokeza kuuza hizi bidhaa kwakuwa zinahitajika sana na watu hivi sasa, wanatumia kujikinga na Corona kwahiyo na sisi tumeona tusikae bure tutumie fursa", amesema, Laizer Molell, muuzaji.

Naye muuzaji mwingine, Idrisa Lubeja amesema, "tumeamua kuichangamkia biashara hii kwa kuwa tumesikia inasaidia kupunguza hatari ya kukumbwa na virusi vya Corona ndiyo maana tumeamua kuichangamkia".

Nao baadhi ya ya wakazi wa jiji la Arusha wamekiri kwamba, kwa sasa limao na tangawizi ni bidhaa muhimu kwao kwani inaaminika kusaidia katika kujifukiza, ikiwa ni njia ya kujikinga na virusi vya Corona.

Aidha tafiti mbalimbali zinadokeza kwamba, utumiaji wa limao kila siku una faida kubwa katika mwili wa binadamu, kutokana na kuwa na virutubisho na madini mbalimbali kama Calcium, Magnesiam, vitamin C, Zink, Potasium, kopa, chuma na Protini.